habari Mpya


Bi.Jane Akabidhiwa Nyumba na Radio kwizera tayari kwa Makazi mapya

NGARA NA GODFREY BISAMBI.
 
Muonekano wa nyumba ya Bi.Janeth Living ambayo imejengwa kwa msaada wa Radio kwizera kupitia wasikilizaji wa kipindi cha Ukumbi wa Matumaini walio jitoa kuchangia ujenzi wa nyumba hiyo.
Ni mkurugenzi wa Radio kwizera fm Padre Fredrick Meela akiongoza sala kwaajili ya kubariki nyumba ya Bi.Jane Living.
  Mkurugenzi wa Radio Kwizera Padre Fredrick Meela akiongoza sala katika tukio la kubariki Nyumba ya Bi.Jane Living, mkazi wa kijiji cha kumunazi wilayani Ngara mkoani Kagera iliyojengwa kwa msaanda wa wadau RADIO KWIZERA kupitia kipindi cha ukumbi wa matumaini

Tukio hilo limefanyika katika kijiji hicho cha Kumunazi liliambatan kukabidhi Nyumba hiyo kwa mama huyo ambaye awali alikua akiishi katika Nyumba iliyochakaa.
Kabla ya kukabidhiwa nyumba hiyo Bi.Jane alikuwa akiisha katika nyumba iliyo kuwa imechakaa mithiri ya Gofu kwani kipindi cha mvua nyumba hiyo ilikuwa ikivuja hali iliyosababisha mama huyo kupatwa na maradhi mabalimbali na kuufanya mwili wake kudhoofu


Hata hivyo kupitia Radio kwizera katika kipindi cha ukumbi wa matumaini wadau mbalimbali walitoa fedha za matibabu ikiwemo fedha kwaajili ya ujenzi wa nyumba hiyo ambayo kwasasa ndio makazi yake mapya.


Aidha Padre Fredrick Meela ameishukuru serikali ya Wilaya ya Ngara chini ya mkuu wa wilaya ya hiyo Luten Kanali Michael Mangwela Mutenjele kwa ushilikiano aliouonesha kwa Radio kwizera kufanikisha ujenzi Nyumba hiyo kutokana na mchango wake alio utoa wa mabati na vifaa vingine.

Post a Comment

0 Comments