habari Mpya


Wananchi Ngara Toeni Taarifa Mapema kwa TAKUKURU kuhusu Miradi ya Maendeleo yenye Harufu ya Ufisadi.

Na Mohamed Makonda –RK Ngara.

Mabalozi 44 wa Kupambana na Rushwa kutoka Kata 22 za wilaya ya Ngara mkoani Kagera wakifatilia elimu ya mapambano dhidi ya Rushwa wakati wa darasa hilo July 1, 2019 kwenye ukumbi wa Community Center mjini Ngara lengo likiwa kwao kuelimisha,kukemea na kuripoti mianya ya rushwa katika kuongeza uwazi na uwajibikaji katika ngazi ya Halmashauri.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, kilichoandaliwa na asasi ya CCRD mkoani Kagera, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Bw Erick Nkilamachumu (pichani katikati) amewataka Wananchi wilayani humo kutoa taarifa mapema kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa miradi ya maendeleo wanaoitilia shaka, kugubikwa na ufisadi ili kuokoa matumizi mabaya ya fedha za umma.

Bw.Nkilamachumu amesema ikiwa wananchi watatoa taarifa mapema , itakuwa ni rahisi kuchukua hatua mapema.

Amsema ni wajibu wa wananchi kushirikiana na viongozi kuanzia ngazi ya kata katika dhana nzima ya maendeleo, ikiwemo kuhoji mapato na matumizi ya miradi iliyomo maeneo yao.

NKILAMACHUMU. 
Awali Mratibu wa Mradi wa TUUNGANE KUTETEA HAKI  kutoka Shirika la CCRD Kagera, Bw Mutayoba Arbogast amesema kwa sababu rushwa ni kosha kisheria na mtu hutumia nafasi au fursa isiofaa kujinufaisha binafsi anaimani elimu waliyoipata Waraghabishi hao wataelimisha jamii, kukemea na kuripoti mianya ya rushwa ili kuongeza uwazi na uwajibikaji ngazi ya Halmashauri mkoani Kagera.


Rushwa inatajwa kuwa ni kikwazo kikuu cha maendeleo ya nchini.ongezeko la vitendo vya rushwa kwenye jamii hupelekea kukosekana kwa utawala bora na uwajibikaji hali inayo-dunisha utoaji wa huduma za jamii,hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya nchini.

Post a Comment

0 Comments