habari Mpya


Radio Kwizera ya ng'ara jijini Johannesburg nchini Afrika ya Kusini

NA AULERIA GABRIEL, JOHANNESBURG
Jumla ya Waandisihi wa habari 42 kutoka nchi 13 za Mashariki na Kusini mwa Afrika, wamekutana mjini Johannesburg nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya namna ya kuandaa na kurusha vipindi na habari zinazohusu mimba za mapema na zisizotarajiwa kwa watoto wa kike.
Mafunzo hayo ambayo yameratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yana lengo la kusaidia kuzuia ama kumaliza tatizo la mimba za mapema na zisizotarajiwa kwa watoto wa wakike katika nchi hizo ambapo kumetajwa kuwa na ongezeko la mimba za utotoni.

Akizungumza katika Ufunguzi wa mafunzo hayo, mshauri wa masuala ua Ukimwi na Afya kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika Bi. Patricia Machawira, amesema mimba za mapema kwa watoto wa kike zimeleta madhara makubwa ikiwemo kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa vijana kutokana na kujiingiza kwenye mapenzi katika umri mdogo.
Pia Bi. Machawira amebainisha kwamba, wasichana wa umri kati ya miaka 15 hadi 19 ndiyo wanaoathiriwa zaidi huku kisababishi kikubwa ikiwa ni umaskini na ukosefu wa malezi bora kutoka kwa wazazi na walezi.


Pichani ni baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiendelea kufuatilia elimu iliyokuwa ikitolewa. 
Mafunzo hayo yameanza jana Julai 29 na yanamalizika Julai 31 mwaka huu ambayo yameshirikisha waandishi wa habari kutoka nchi za Afrika Kusini, Tanzania, Namibia, Zambia, Uganda, Kenya, Mozambique, Lesotho, Ethiopia, Zimbabwe, Malawi, Botswana na Eswatini.


Pichani ni Mwandishi na mtangazaji wa Radio kwizera fm ambaye pia ni Mhariri mkuu wa Radio kwizera Bi.Auleria Gabriel akifuatilia mafunzo hayo. 

Tanzania imewakilishwa na waandishi sita ambapo wanne wametoka Tanzania na wawili kutoka kisiwani Zanzibar. Waandishi hao ni Auleria Gabriel (Radio Kwizera), Lulu Mzee Mohammed (ZBC), Theresia Thomas Kiyombibi (Mazingira FM), Anna Mwasyoke (TBC) Gaspary Gaspary Charles (Micheweni FM) na Syriacus Mukuzi (The Citizen).
 

Post a Comment

0 Comments