![]() |
Mkuu wa Wilaya
ya Buhigwe Mkoani Kigoma Kanali Michael
Ngayalina kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama amezindua Benki
ya matofari katika kijiji cha Kitambuka, Kata Mukatanga kwa ajili ya ujenzi wa
miundombinu itakayowezesha utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.
Uzinduzi huo
umefanyika katika kata hiyo kufutia Kata ya Mukatanga yenye vijiji Vitatu
kukosa kituo cha afya jambo linalopelekea wananchi kusafiri umbali mrefu
kufuata huduma za matibabu.
Nao wananchi
walioshiriki katika uzinduzi huo wamesema kutokana na usumbufu wa kusafiri
umbali mrefu kufuata huduma za afya wameazimia kwa pamoja kujenga kituo cha
afya na kuiomba serikali kuunga mkono jitihada zao.
SIKILIZA ZAIDI HAPA CHINI
|
0 Comments