habari Mpya


Wananchi Kijiji cha Buhororo Ngara Wamfukuza Mwalimu Shule ya Msingi Wakimtuhumu kwa Ushirikina.

Mkutano wa Kijiji Ukiendelea. 

Serikali na Wananchi wa kijiji cha Buhororo, Kata ya Kibimba wilayani Ngara mkoani Kagera kwa kauli moja wamekataa kufanya kazi na Mwalimu Paulina Joseph wa shule ya msingi Buhororo huku wakimtaka aondoke kijijini humo kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kishirikina

Uamuzi huo umefikiwa leo June 6,2019 na Wananchi  hao pamoja na Viongozi wa kijiji kupitia mkutano wa kijiji, baada ya kudaiwa kuwa Walimu 14 wa shule ya msingi Buhororo wanataka kuhama kwenye shule hiyo ikiwa halmshauri itashindwa kumuondoa mwalimu huyo ambaye amekuwa akiwasumbua kishirikina walimu wenzake pamoja na wananfunzi.

WASIKILIZE HAPA WAKAZI WA BUHORORO.
Mara baada ya kusikiliza malalamiko ya wananchi na walimu, Mwenyekiti wa kijiji cha Buhororo Bw.Staphod Simon amesema ipo haja ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ngara kumuondoa Mwalimu Paulina Joseph katika shule hiyo kabla ya shule kufunguliwa kwani huenda wananchi wakajichukulia sheria mkononi na kumdhuru.

KAULI HAPA CHINI  YA MWENYEKITI BUHORORO.

Kwa upande wake mtuhumiwa Mwalimu Paulina Joseph, alipotafutwa na Redio Kwizera mara baada ya mkutano huo amesema tuhuma anazobebeshwa si za kweli kwani hakuna mtu mwenye ushahidi way eye kujihusisha na vitendo hivyo.
UTETEZI WA MWALIMU ANAYETUHUMIWA.
Hata hivyo Mkurugenzi wa halmashauri ya Ngara Bw. Aidan Bahama amesema hajapata taarifa za tuhuma juu ya Mwalimu Paulina lakini ameahidi kulifuatilia na kuchukua hatua

Post a Comment

0 Comments