habari Mpya


Uhuru usio na mipaka kwa watoto wa kike unaotolewa na baadhi ya wazazi umetajwa kuwa chanzo cha kesi za ukatili kuendelea kuripotiwa

NGARA:Na Erick Ezekiel
Uhuru usio na mipaka kwa watoto wa kike unaotolewa na baadhi ya wazazi umetajwa kuwa chanzo cha kesi za ukatili kuendelea kuripotiwa katika baadhi ya maeneo na kusababisha jinsia ya kike kuendelea kutafrisiwa kuwa dhaifu ndani ya jamii.


Hayo yamesemwa na Afisa afya wilaya ya Ngara Bw. Mansour Kalokola wakati akizungumza na wakazi wa vijiji vya Nyabihanga na Bukirilo wakati wa tamasha la kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, kupinga ukatili wa kijinsia pamoja na elimu ya kuboresha afya na usafi lililoandaliwa na Shirika la Tanganyika Christian Refugee Service (TCRS) wilayani Ngara.

Amesema baadhi ya wasichana hujikuta wakikatiza masomo na kuanza majukumu ya uzazi licha ya kuwa wamepelekwa shule kwa ajili ya kusoma hivyo ipo sababu ya familia kuzingatia malezi bora ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza na kuwashauri watoto wa kike juu ya hali ya maisha.

Awali mratibu wa TCRS wilaya ya Ngara Bw. Peter Mwaitege amesema shirika hilo kama sehemu ya jamii kupitia matamasha linahamasisha wananchi juu namna bora ya kutunza mazingira na kuboresha afya hasa katika maeneo yenye miradi inayofadhiliwa na shirika hilo.

Post a Comment

0 Comments