habari Mpya


Soma Habari -Kunyongwa hadi Kufa Karagwe na Kufungwa Jela Miaka 30 Ngara kisa Kilimo cha Bangi.

Source; RK: EM (WATU WANNE KUNYWA HADI KUFA)
ED: AG
Date: Friday, June 07, 2019

KARAGWE

Mahakama kuu ya Tanzania iliyokaa kwa ajili ya kusikiliza kesi za mauaji chini ya Jaji Edisoni Mkasimongwa imewahukumu watu wanne kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya mauaji.

Wakili wa serikali Bw. Juma Maona amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Byamtozi John, Isaya Venant wakazi wa kijjiji cha Kishao wilayani Karagwe pamoja na Dastani Makwaya na Jovith Mtaganywa wakazi wa kijiji cha Kagenyi wilayani Kyerwa.

Amesema kuwa Byamtozi John na Isaya Venant mnamo Agosti 6, 2011 walimuua Bw. Aprolo Eliasi huku watuhumiwa Dastani Makwaya na Jovith Mtagaywa mnamo Juni 17, 2013 walimua Oscar Matin mkazi wa kijij cha Kagenyi wilayani Kyerwa.

Jaji Mkasimogwa amesema kuwa mahakama imetoa adhabu hiyo ili iweze kuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

Source; RK: SD (mahakamani)
ED: AG
Date: Friday, June 07, 2019

NGARA

Raia mmoja wa Burundi amehukumiwa na mahakama ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera kifungo cha miaka 30 baada ya kukiri kosa la kupatikana na hatia ya kujihusisha na kilimo cha Bangi na kuingia nchini kinyume cha sheria.

Akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Ngara Endrew Kabuka amesema kuwa mahakama inatoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia ya kulima dawa za kulevya kinyume cha sheria.

Awali mwendesha mashitaka wa Polisi Respiusius John, amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Erick Higirukwishaka raia wa Burundi ambaye amekamatwa June 02 katika kijii cha Mumasama kata ya Ngara mjini akiwa amelima miche 115 ya Bangi katika shamba lake.

Mtuhumiwa baada ya kufikishwa mahakamani alikuwa akikabiliwa na mashitaka mawili moja likiwa la kujihusisha na kilimo cha bangi na kosa la pili kuingia nchini kinyume cha sheria ambapo alikiri kosa la kwanza huku kosa la pili akikana.

Hata hivyo, Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani June 17 mwaka huu kujibu shitaka la kuingia nchini kinyume cha sheria.

Post a Comment

0 Comments