habari Mpya


Radio Kwizera ya fanikisha ujenzi wa nyumba ya Bi.Jane mkazi wa wilaya ya Ngara aliyeishi katika mazingira magum kwa muda mrefu bila msaada

NGARA: Na Godfrey Bisambi
Pchani kushoto ni mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera  Luteni Kanali Michael M. Mtenjele akikabidhi mabati kwa Bi.Jane Living wakwanza kulia


Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Luten Kanali Michael M.Mtenjele na mkurungenzi wa Radio kwizera Padre Fredriki Meela wakikabidhi vifaa vya ujenzi kwa mama mkazi wa kijiji cha kumunazi wilayani Ngara mkoani Kagera.
vivfaa hivyo vya ujenzi vimepatikana kupitia Juhudi za Radio kwizera kupitia kipindi cha ukumbi wa matumaini kinachoendeshwa na Sister Oliva Niyonzima mtangazaji wa Radio kwizera.


Mama huyu ni Jane Living ambaye anaisha katika mazingira magum na ameugua kwa muda mrefu bila msaada ambapo Sister Oliva amemuibua kupitia kipindi cha ukumbi wa Matumaini kinachorushwa na Radio Kwizera kila jumanne saa nne usiku hadi saa saba usiku, Radio Kwizera kwa kushirikiana na wasikilizaji wamemjengea boma la nyumba ya vyumba vitatu ambapo mkuu wa wilaya ya Ngara Luten Kanali Michael M.Mtenjele ametoa Mabati ya kuezeka nyumba hiyo na misumariKupitia tukio hilo mkuu wa wilaya ya Ngara ametoa pongezi kwa mkurungenzi wa Radio kwizera kwa kujitoa kama mkuu wa kituo na kuruhusu kipindi kurusha vipindi vya kuisaidia jamii katika matatizo mbalimbali yanayoikumba jamii ya kitanzania.Aidha Luteni Kanali Mtenjele amempongeza pia Sr.Oliva Niyonzima kwa kazi ngumu anayoifanya kwa moyo na kumsihi aendeleze moyo huo huo wa kujitoa kuisaidia jamii
Pichani kulia aliyeshika Baisikeli ni Mkurugenzi wa Radio kwizera fm Padre Fredrick Meela akisaidia kumpandisha Bi.Jane Living Kwenye baiskeli baada ya magari kushindwa kufika eneo la tukio


Mkuruganzi wa radio kwizera akizungumzia tukio hilo amesema Radio kwizera itaendelea kuwa karibu na wasilkilizaji wake wote bila kubagua na itakua msitari wa mbele kuisaidia jamii.

Mkuu wa wilaya ya ya Ngara Luteni Kanali Michael M.Mtenjele na Mkurugenzi wa Radio kwizera Padre Fredrick Meela wakishiriki ujenzi katika nyumba ya Bi.Jane Living
 

Post a Comment

0 Comments