habari Mpya


Mkuu wa wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma atoa tahadhari juu ya ugonjwa wa Ebola

 KIBONDO: Na,James Jovin. Picha na Maktaba yetu
Mkuu wa wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma Bw.Luis Bura amewatahadharisha wananchi wa wilaya hiyo juu ya ugonjwa wa Ebola unaoelezwa kuwepo katika nchi za DRC na Uganda kwa kuwa wilaya hiyo iko mpakani


Bw.Bura ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kueleza kuwa wananchi wanapaswa kutoa taarifa mapema juu ya viashiria vyovyote vya ugonjwa wa ebola iwapo vitatokea

Aidha amewataka wafanyabiashara wanaotoka katika wilaya ya Kibondo na kwenda katika nchi za Uganda na Congo kuwa makini na kuhakikisha wanafanyiwa vipimo kabla ya kurejea nchini

Hata hivy mkuu wa wilaya ya Kibondo amewahakikishia wakaazi wa wilaya hiyo kuwa mpaka sasa hakuna mtu yeyote anayeonekana kuwa na dalili za Ebola na hatua madhubuti za kudhibiti ugonjwa huo tayari zimechukuliwa

Post a Comment

0 Comments