habari Mpya


Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, "Amani Yetu Tuendelee Kuitunza".

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma Kanali Michael Masala Ngayalina amezungumza na Waumini wa Kiislam na Viongozi mbali mbali wa dini nyengine kwenye TAFRIJA Kubwa ya IFTAR iliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya Pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama.

"Pamoja na kuwepo kwa dini zetu tofauti, dini ya Kiislam na dini nyengine nchi mwetu Tanzania, tuendelea kujivunia Hali yetu ya kuvumiliana Pamoja ili tuendelee kutunza Amani yetu. Uislam neno hili Lina maana ya Amani. 

Na Leo hii tumekusanyika kwa Pamoja haijalishi ni dini gani tunafuturu kwa pamoja na furaha. Ni ishara tosha kuwa tunapendani. Upendo huu ndio chanzo kikubwa cha Amani yetu."

Pamoja na Tafrija hii , Mkuu wa Wilaya Kanali Michael Masala Ngayalina aliambata na Viongozi wa Wilaya BAKWATA Katika kufanisha IFUTARI hiyo.
 
" Nipende kutumia FURSA HII kuwakumbusha Tena mwezi wa Ramadhani ni mwezi mwema unapoisha tunatakiwa kuishi kwa kumcha Mungu ili tufanikiwe. Hivyo basi tunapojinda na sikukuu ya Eid el Fitr tunapaswa kusherehe kwa Amani". 
 
Katika iftar hiyo waislam walimuomba , Mkuu wa Wilaya mambo makuu matatu kwa maendele ya wilaya. Mambo hayo ni changamoto kubwa zinazokikabili jamii ya Wilaya ya Buhigwe kwa ujumla.

i. Kuomba kuwa na eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya kuzikia.

ii. Kuomba kuwepo kwa eneo maalum kwa ajili ya machinjio Wilayani

iii. Kuomba ukubwa wa eneo wa hekari 10 kwa ajili ya kujenga chuo cha ufundi kitachotoa elimu ya ufundi kwa jamii yote ya wana buhigwe. 
Iftar ili kamalika kwa Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe kuongea na waislamu pamoja na wageni waalikwa,kwa kuwasilisha ahadi ya fedha taslimu shilingi laki moja kati ya shilingi laki mbili za waislamu wa Buhigwe zilizoahidiwa kwenye Harambee ya ununuzi wa vyombo vya usafiri kwa ajili ya Jeshi la Polisi wilayani humo ili kuunga juhudi na jitihada ya  Mkuu wa Wilaya Katika kuliwezesha Jeshi la Polisi Katika kufanya kazi vizuri, Pia Sheikh wa Wilaya ya Buhigwe aliwaongoza wageni waalikwa kwenye kuliombea Taifa letu Amani Pamoja na kumpongeza  MKUU WA WILAYA kwa jambo alilolifanya, Kwani halikuwahi kufanyika hapo awali.

Post a Comment

0 Comments