habari Mpya


Kuelekea AFCON 2019 - Taifa Stars Yafungwa 1-0 na Misri.

Nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta akimtoka beki wa Misri, Mahmoud Alaa ambapo katika mchezo huo wa kirafiki wa Kimataifa Jana June 13, 2019 , Tanzania ilichapwa bao 1-0 na wenyeji, Misri katika Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.

Goli la wenyeji kwenye mchezo huo maalum kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2019) zinazotarajiwa kuanza Juni 21 hadi Julai 19,2019 nchini Misri limefungwa na kiungo wa Aston Villa ya Uingereza, Ahmed El Mohamady dakika ya 64.
Pamoja na kufungwa, Taifa Stars inayofundishwa na Emmanuel Amunike, atafanya uchunguzi wa kutosha katika kikosi chake na atakifanyia marekebisho kuelekea kuanza kwa fainali za AFCON 2019, Tanzania imepangwa Kundi C na timu za Senegal, Kenya na Algeria.

Taifa Stars itacheza mechi zake tatu za Kundi C AFCON 2019 dhidi ya Senegal Juni 23, Kenya Juni 27 na Algeria Julai 1,2019 .

Misri wapo Kundi A pamoja na Zimbabwe, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Kundi B linaundwa na Burundi, Madagascar, Guinea na Nigeria, Kundi D linaundwa na Namibia, Afrika Kusini, Ivory Coast na Morocco, wakati Kundi E kuna Angola, Mauritania, Mali na Tunisia na Kundi F ni Guinea Bessau, Benin, Ghana na mabingwa watetezi,
Cameroon. 

Post a Comment

0 Comments