habari Mpya


Kasulu Walia na Bei Kubwa ya Mifuko Mbadala.

Mifuko Mbadala.

Baadhi ya wafanyabiashara wa halmashauri ya mji wa Kasulu Mkoani Kigoma wameiomba serikali kupunguza bei ya mifuko mbadala iliyoletwa baada ya katazo la kutumia mifuko ya plastiki nchini kulingana na hali ya uchumi wa wananchi.

Wakizungumza na radio kwizera mjini Kasulu wamesema kwa sasa wamepoteza wateja wao wa awali kutokana na mifuko mbadala kutokuwa imara huku bei yake ikiwa ni kubwa kuliko bidhaa zinazonunuliwa.

Wamesema Serikali inapaswa kufikiri njia mbadala ya kutengeneza mifuko iliyo imara na yenye bei nafuu kulingana na uchumi wa wananchi ili kukidhi mahitaji ya wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.

WANANCHI JUU YA MIFUKO MBADALA.

Akijibu malalamiko ya Wananchi hao Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kasulu Bi Fatuma Laai amesema ofisi yake kupitia idara ya maendeleo ya jamii wameanza kuelekeza vikundi mbalimbali vinavyokopa mikopo halmashauri kutumia mikopo hiyo kutengeza kiwanda cha mifuko imara ili kutatua changamoto zinazotokana na mifuko hiyo.

Post a Comment

0 Comments