![]() |
Serikali
nchini imemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara na Afisa Elimu Sekondari
kukutana na umoja wa vijana wa vyuo vikuu nchini wanaotoka wilayani Ngara
mkoani Kagera ambao wamekuwa wakijitolea kufundisha katika shule za sikondari
ili kuwawezesha.
Kauli hiyo
imetolewa Bungeni Jana June 10, 2019 jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe.Mwita Waitara wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Ngara Bw.Alex Raphael Gashaza.
Katika swali
lake la Nyongeza, Mbunge Gashaza amehoji
Vijana wanao soma
vyuo vikuu nchi nzima wanaotoka wilayani Ngara kwa miaka miwili mfululizo
wakati wa likizo ndefu wamekuwa wakijitolewa kufundisha katika shule za
sekondari, je serikali haioni sababu ya kuwaunga mkono katika kazi hiyo.
…….GASHAZA.
Katika
majibu yake Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe.Mwita
Waitara amesema kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara na Afisa Elimu
Sekondari wanapaswa kufanya mazungumzo na vijana hao kujua nini wanahitaji ili
serikali iwaunge mkono.
…….WAITARA.
|
0 Comments