habari Mpya


Yanga SC Yakaa Kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2018/2019.

Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting umewafanya Yanga SC kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2018/2019.

Mechi hiyo iliyochezwa May 14, 2019 Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam, unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 83 baada ya kucheza mechi 36, sasa ikiwazidi pointi moja, mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 82 ambao hata hivyo wana mechi tatu mkononi ikiwemo ya Mtibwa Sugar watakayocheza May 16, 2019.

Katika mchezo huo bao pekee la Yanga SC lilifungwa na kiungo Papy Kabamba Tshishimbi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dakika ya 15.

Matokeo ya mechi nyingine ya Ligi Kuu , Mwadui FC imelazimishwa sare ya 3-3 na Mbao FC ya Mwanza Uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga.

Mabao ya Mwadui FC yamefungwa na Ottu Joseph mawili, dakika za 46 na 69 na Gerald Mathias dakika ya 58, wakati ya Mbao FC yamefungwa na Abubakar Ngalema dakika ya 35, Said Junior dakika ya 44 na Hamim Abdul dakika ya 86.

Post a Comment

0 Comments