habari Mpya


Wazazi wa Kiume Kibondo Hudhurieni Kliniki na Wenza wenu Mpate Elimu ya Lishe.

Na James Jovin –RK Kibondo.

Jumla ya Wazazi na Walezi elfu 48 mia 856 wanaohudhuria kliniki ya Baba Mama na Mtoto wilayani Kibondo Mkoani Kigoma wamepata elimu ya lishe ikiwa ni mkakati wa kutokomeza utapiamlo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Afisa Lishe Wilaya ya Kibondo Bw Tumaini Muna amebainisha hayo wakati wa kikao cha kamati ya lishe kilichofanyika katika ukumbi wa IOM na kuongeza kuwa shughuli hiyo imefanyika katika vituo vya afya na zahanati zote zinazotoa huduma ya kliniki ya baba, mama na mtoto.

Amesema elimu hiyo imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza maradhi na changamoto mbali mbali zinazowakabili watoto walio chini ya miaka mitano.

Bw Muna 

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Lishe wilaya ya Kibondo Dr. Gabriel Chitupila amewataka Wazazi na Walezi hasa Wanaume kujenga tabia ya kuhudhuria kliniki wakiwa na Wenza wao ili kupata elimu kuhusu afya itakayosaidia familia kufuata kanuni bora za afya.

Post a Comment

0 Comments