habari Mpya


Wanafunzi wenye Mazingira Magumu Muleba Wapewa Vifaa vya Shule.

Na Shafiru Yusuf – RK Muleba.


Vifaa  vya shule vyenye thamani ya zaidi ya milioni 4 na laki 9

vimegawiwa  na halimashauri ya Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera kwa

wanafunzi 100 wa shule za msingi na sekondari ambao wanaishi mazingira

magumu na  hatarishi ili waweze kuongeza kiwango cha taaluma.

Akizunguza na Redio Kwizera baada ya kugawa vifaa hivyo afisa

maendeleo ya jamii ambaye pia ni mratibu wa kudhibiti Ukimwi Wilaya ya

Muleba Bi. Enrietha William amesema vifaa hivyo ni kalamu, daftari,

sare za shule na rula ambapo vimegawiwa kwenye shule 67 za msingi na

sekondari.
Bi. William amesema kuwa lengo la kugawa vifaa hivyo kwa wananfunzi

hao ni kuinua kiwango cha taaluma kutokana na baadhi yao kuishi

mazingira ambayo yanawafanya kushindwa kumudu gharama za kununua vifaa

hivyo hali ambayo inapelekea kusindwa kuendelea na masomo yao.Baadhi ya Walimu wilayani Muleba wamesema licha ya kutopewa wanafunzi

wote wanaoishi mazingira magumu vifaa hivyo, wameishukuru Halmashauri 

ya Wilaya ya Muleba kwa kugawa vifaa hivyo ambavyo

vitaweza kuinua kiwango cha taaluma mashuleni.Kwa upande wao baadhi ya Wanafunzi Wilayani humo wamesema tatizo la

ukosefu wa vifaa vya shule kwao, 

 imechagia ungezeko la utoro kwa wananfunzi kutokana na baadhi

yao hushindwa kuendelea na masomo kwa kukosa gharama za kununua vifaa

hivyo.

Post a Comment

0 Comments