habari Mpya


TCRA na Usajili wa Line za Simu May 01,2019.

Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA,Kanda ya Ziwa Leo imetoa ufafanuzi kuhusu Utaratibu wa Kusajili Line za Simu kwa kutumia alama za vidole na Kusema kuwa Mwananchi anatakiwa kukumbuka namba ya kitambulisho Cha taifa inayotolewa na NIDA kabla ya Kupewa kitambulisho hicho.

Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo ametoa Kauli hiyo alipo kuwa akizungumza na Waandishi wa  Habari katika Ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya ziwa zilizopo Jijini Mwanza na kusema kuwa sio lazima Mwananchi akasubiri kupata kitambulisho ndipo asajiliwe bali ni namba pekee ya utambulisho inayotolewa na nida wakati akisubiri kupewa kitambulisho cha taifa.

 - MIHAYO

Kwa Undani wa Taarifa Hii Usikose Kusikiliza Kipindi Cha Asubuhi Njema Hapa Radio Kwizera Fm Leo May 01,2019 ili kupata Ufafanuzi zaidi kuhusu Usajili wa Line za Simu kwa kutumia alama za Vidole.

Post a Comment

0 Comments