habari Mpya


Taarifa ya Habari Saa 24 Zilizopita Radio Kwizera FM.

Source; RK: SY (kujinyonga)
ED: FM
Date: Thursday, May 23, 2019

MULEBA 

Mtu mmoja Mkazi wa Kitongoji cha Kagabiro kata ya Muleba Wilayani Muleba Mkoani Kagera amekutwa amejinyonga Kwa kutumia kamba ya nailoni Nyumbani kwake huku chanzo cha kujinyonga bado hakijajulika

 Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Bw Gabriel Rwakabwa amemtaja marehemu kuwa ni Ponsian Rusigazi anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 59 ambapo tukio hilo limetokea jana

Bw Rwakabwa amesema amepewa taarifa na wananchi juu ya tukio hilo ndipo akafika eneo la tukio na kukuta  Ponsian akiwa amening’inia juu ya paa la nyumba yake ndipo akatoa taarifa kwa jeshi la polisi

Hata hivyo jeshi la polisi Wilayani humo limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuruhusu mwili wa marehemu kufanyiwa maziko huku likiwataka wananchi kutojichukulia sheria mkononi

Source; RK: EZ (upimaji wa VVU)
ED: FM
Date: Thursday, May 23, 2019

NYANGHWALE
Zaidi ya asilimia themanini ya wakazi wa Wilaya ya Nyangh’wale Mkoani Geita waliojitokeza kupima maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa hiari 2018/2019, wamebainika kuwa na VVU 

Mratibu wa kudhibiti kifua kikuu na ukimwi wilayani humo Dk Darius Nyanda akiongea na radio kwizera ofisini kwake , amesema moja ya njia iliyofanikisha mwitikio huo ni pamoja na zoezi la tohara kwa wanaume.

Dk Nyanda ameeleza kuwa licha ya kufikia mafanikio hayo bado wilaya hiyo ina changamoto ya idadi kubwa ya wananchi ambao hawazifahamu hali zao kiafya.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi Wilayani humo waliopima na kugundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi wamesema dawa wanazopatiwa zimewasaidia kwa kiasi kikubwa na mpaka sasa wanaendelea na shughuli za kiuchumi kama kawaida.


Source; RK: AJ (maadili)
ED: FM
Date: Thursday, May 23, 2019

KAKONKO
Zaidi ya viongozi 30 wakiwemo viongozi wa umma na viongozi wa siasa Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma wametakiwa kuzingatia misingi ya maadili na kuheshimu miiko ya uongozi. 
Wito huo umetolewa na Afisa Kamati ya Maadili kanda ya magharibi Bw Onesmo Msalangi akitoa mafunzo ya maadili kwa viongozi waumma na siasa wilayani humo.
 Bw Msalangi ameongeza kuwa baadhi ya miradi ya maendeleo imeshindwa kukamilika katika maeneo mbalimbali kutokana na kukosekana uadilifu na maadili kwa baadhi ya viongozi katika maeneo yao
Kwa upande wao baadhi ya viongozi walio patiwa mafunzo hayo wameahidi kuyazingatia huku wakieleza kuwa watakuwa mabarozi na wasimamizi wa maadili katika ofisi zao hali itakayo saidia kuimarisha utendaji kazi na uwajibikaji


Source; RK: AE (Ukosefu wa maji)
ED: FM
Date: Thursday, May 23, 2019

KIGOMA
Wananchi wa kata ya Bitale halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Mkoani Kigoma wamelalamikia ukosefu wa barabara zinazounganisha vijiji vya kata hiyo sambamba na huduma ya maji safi na salama hali inayohatarisha usalama pamoja na afya zao .

Wakizungumza na Redio Kwizera juu ya changamoto hizo, wananchi hao wamesema kwa muda mrefu wanatumia maji ya mito na mvua licha ya kuwa vijiji vyao vimeunganishwa katika mradi mkubwa wa maji Mkongoro 

INSERT………..WANANCHI
Diwani wa kata ya Bitare Bw Mathias Bwami amesema serikali imeweka mikakati ya kumaliza changamoto ya maji katika kata hiyo na kwamba tatizo hilo linatokana na kukosekana kwa fundi anaetakiwa kufanya kazi ya kufunga na kufungua mabomba ya maji.

Post a Comment

0 Comments