habari Mpya


Simba Yatafuna Miwa ya Mtibwa Ligi Kuu.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba SC wamerejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya jana May 16,2019 kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, kwenye Dimba la Uhuru Dar es Salaam.


 Walioitafuna miwa ya Mtibwa kwenye mchezo huo uliokuwa mzuri na wa kuvutia, ni John Bocco dakika ya 33, Clatous Chama dakika ya 48 na Emmanuel Okwi dakika ya 56.

Ushindi huo umefanya Simba SC ifikishe pointi 85 na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwaacha Yanga SC kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 83 wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 49 baada ya kucheza mechi 36, ikibaki nafasi ya tano na KMC yenye pointi 49 pia za mechi 36.

Wachezaji Emanuel Okwi wa Simba na Casian Ponera wa Mtibwa Sugar wamezungumzia matokeo ya mchezo huo.

Post a Comment

0 Comments