habari Mpya


Simba SC na Pointi 21 za TPL Bingwa 2018/2019.

Timu ya Simba SC imefanikiwa kuibuka na ushindi baada ya kupata bao zikiwa zimebaki sekunde chache mpira kumalizika kupitia kwa Hassan Dilunga.

 Bao la Simba SC limefungwa ndani ya dakika 7 za nyongeza (90’+7) na kuendelea kuwasogelea Yanga SC ambao wanaongoza Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi 77 na michezo 33, huku Simba SC ambao wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 72 na michezo 28, mbele ya Azam FC waliopiga April 29,2019 na Yanga SC na kubaki nafasi ya tatu wakiwa na pointi zake 66 na michezo 33.


Kimsingi Yanga SC hadi sasa anatafuta point 15 wakati Simba SC anawania pointi 30, Yanga SC kama atashinda michezo yake yote mitano atapata pointi 15 hivyo atamaliza Ligi akiwa na jumla ya pointi 92, wakati Simba SC akishinda mechi zote 10 atamaliza Ligi akiwa na pointi 102, hivyo Simba SC anahitaji ushindi katika mechi 7 (Point 21) pasipo kujali matokeo ya timu yoyote ili awe Bingwa kwani atakuwa ana point 93 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.

Post a Comment

0 Comments