habari Mpya


Kero ya Taka Mjini Geita.

Picha/Habari na Gibson Mika –RK Geita 90.5

Baadhi ya wakazi wa halmashauri ya mji wa Geita mkoani Geita wameilalamikia halmashauri ya mji huyo kutozoa taka kwa wakati  ndani ya  vifaa maalumu vya kutunzia taka (pichani) vilivyopo pembezoni mwa barabara kuu  ya Geita hali inayosababisha kuwepo kwa harufu mbaya.
Wakizungumza katika  mkutano wa hadhara uliowakutanisha Wananchi, Viongozi wa halmashauri hiyo na Mkuu wa mkoa huo, Mhandisi Robart Gabriel wamesema mpango wa halmashauri ya mji wa Geita wa  kuweka vifaa maalumu vya kutupia taka pembezoni mwa barabara ni  mzuri lakini  changamoto kubwa ni kutozolewa kwa wakati.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Mji wa Geita Adolph Ritte amesema changamoto kubwa iliyojitokeza na kushindwa kuzoa uchafu kwa wakati ni baada ya usafiri uliokuwa ukitumika kukusanya taka hizo  kuharibika na kwamba hadi sasa halmashauri hiyo imefanikiwa kuleta trekta tatu, na magari matatu aina ya lori hivyo kero hiyo itatatuliwa.

Hata hivyo,  mkutano huo umefanyika muda mfupi baada ya mwandishi wa radio kwizera Mkoani  Geita kuripoti moja kwa moja kwenye kipindi cha mchakato kuhusu mrundikano wa taka hizo kwenye barabara za mji wa geita huku zikiwa zimejaa kwenye vifaa hivyo bila kuondolewa.

Post a Comment

0 Comments