habari Mpya


Zahanati ya Nyankere, Missenyi mkoani Kagera Yateketea Kwa Moto bila Kuokoa kitu Chochote.

Muonekano wa Mabaki ya vifaa mbalimbali vya Zahanati ya Nyankere iliyopo Kata Mabale wilayani Missenyi mkoani Kagera ikiwaimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia April 3,2019 huku chanzo cha tukio hilo kikiwa bado hakijajulikana.

Mkuu wa wilaya ya Missenyi Kanal DENIS MWIla amesema kuwa tukio hilo limetokea saa nne usiku nakwamba moto huo umeshindwa kuzimwa kutokana na kutegemea kikosi cha zima moto na uokoaji kutoka Bukoba ambapo hadi wanafika wamekuta moto tayari umeteketeza zahanati hiyo.
Amesema uchunguzi wa kutambua chanzo halisi cha moto huo na tathimini ya mali zilizoteketea unaendelea na utakapokamilika itatolewa taarifa kamili.
 
Hata hivyo halmashauri ya wilaya ya Missenyi imesema kuwa itajenga Mahema kwa ajili ya kutolea huduma muhimu za afya hasa za mama wajawazito na watoto.

SIKILIZA ZAIDI HAPA CHINI.

Post a Comment

0 Comments