habari Mpya


Wavuvi Kagera zingatieni Ubora Katika Uchakataji wa Mazao ya Samaki au Dagaa.

Mjasiriamali katika visiwa vinne vya Kimoyomoyo, Mulumo, Kassenyi, na Chakazimbwe katika Kata za Mazinga na Ikuza wilayani Muleba mkoani Kagera akichakata dagaa kwa uanikaji ili kuowaongezea thamani na kuuza katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Wataalamu wa uchumi wanabainisha uanikaji dagaa chini kuwa hauruhusiwi kufanya hivyo kwani dagaa wakianikwa chini kwenye mchanga ubora wake unapungua katika masoko ya ndani na yale ya nje ya nchi. 

Dagaa hao huwa na mchanga jambo ambalo huleta usumbufu mkubwa kwa watumiaji.
Akifanya ziara ya siku mbili Machi 28 hadi 29, 2019 ,Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Profesa Faustin Kamuzora katika kusimamia maendeleo ya mkoa kupitia sera ya kila mwananchi kujikwamua kiuchumi kwa kuzalisha na kujiingizia kipato halali kupitia kazi anayoifanya alitembelea na kukagua miradi ya maendeleo Visiwani Wilayani Muleba na kuongea na wavuvi kwa kuwaelimisha juu ya uvuvi wa kisasa wenye tija na kukuza uchumi.
Katika mikutano yake na wananchi waishio visiwani Prof. Kamuzora mara baada ya kutembelea na kukaua miradi ya maendeleo aliwaelimisha wananchi hao kuzingatia ubora wa mazao wanayoyazalisha hasa ubora wa samaki au dagaa wanapochakatwa kabla ya kufikishwa sokoni.

 Hapa nchini Tanzania tuna tatizo kubwa la uharibifu baada ya mavuno (Post Harvest Loss) yaani unakuta mwananchi anahangaika kuzalisha bidhaa zake ili akauze sokoni lakini anashindwa kuziandaa bidhaa hizo katika hatua za mwisho wakati wakuzipeleka sokoni jambo ambalo linapelekea hasara kubwa kwa mhusika na wakati mwingine kusababisha madhara kwa watumiaji.” Alitahadharisha Prof. Kamuzora

Prof. Kamzora aliwaagiza Maafisa Uvuvi na Maafisa Afya visiwani humo kuhakikisha wanatekeleza sheria ya uvuvi Namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009 katika kusimamia masuala ya uvuvi na uchakataji wa mazao yake na kuchukua hatua kali kwa wale wote ambao wanaoendelea kukiuka sheria, taratibu na kanuni za uvuvi.
Mwisho Prof. Kamzora aliwataka Wavuvi Mkoani Kagera kuachana na uvuvi haramu au kutumia zana haramu katika kuvua ambapo alichoma nyavu haramu katika kisia cha Chakazimbwe, wilayani ya Muleba

Post a Comment

0 Comments