habari Mpya


Wanafunzi Biharamulo:Falsafa ya Mwalimu Nyerere Haitekelezeki kwa Misingi ya Uzalendo.

Na William Mpanju RK Biharamulo.

Baadhi ya Wanafunzi wa Kidato cha nne na sita katika Shule ya Sekondari  Ruziba na Kagango  wilayani Biharamulo Mkoani  Kagera  wameitaka  serikali kuimarisha  kigoda cha mwalimu Julias  Nyerere kama sehemu ya kuenzi  falsafa ya  maadili, utawala bora na demokrasia  kwa kizazi kilichopo na kijacho.

 Wanafunzi  hao wamesema  hayo wakati wa mdahalo wa kigoda  cha mwalimu  Nyerere  kilichozinduliwa  April 19, 2019 katika wilaya hiyo,kwa kuwashirikisha  baadhi ya wanafunzi shule za sekondari   pamoja  na walimu wakuu wa  shule ya Rubondo ,Ruziba  na Kagango.
James  Matiko , Lisa  Revocatus  na Honorata  Stanslaus  wamesema  falsafa  ya Mwalimu Nyerere  haitekelezeki  kwa  misingi ya uzalendo  kutokana kuwa maadili ya baadhi ya watumishi wa serikali hairidhishi.

WASIKILIZE HAPA CHINI.   

Post a Comment

0 Comments