habari Mpya


Unaupotevu wa Chochote? Soma Hapa Taarifa ya Jeshi la Polisi Makao Makuu.

Jeshi la Polisi nchini kupitia kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa kushirikiana na Government e-Payment Gateway (GePG) limeanzisha mfumo wa upatikanaji wa fomu ya upotevu (Police Loss Report) kupitia mtandao wa https://Lormis.tpf.go.tz  na kufanya malipo kwa njia ya simu kwa mfumo wa  GePG. 
 
Mfumo huo ulianzishwa  mwezi Machi, 2019 na kitengo cha TEHAMA Makao Makuu ya Polisi  kwa lengo la kupunguza gharama na kurahisisha upatikanaji wake katika vituo vya Polisi  humuwezesha mtu yeyote kufanya maombi na malipo ya Loss Report kwa njia ya mtandao na baadaye mwombaji  kwenda Kituo cha Polisi ili kukamilisha huduma hiyo.

Mwombaji wa fomu ya upotevu kwa njia ya mtandao, atatakiwa kufuata hatua zifuatazo:-
  1.  Kujaza fomu kupitia mtandao wa https://lormis.tpf.go.tz/ na kutoa maelezo ya upotevu
  2.   Akisha jaza fomu hiyo atapatiwa ‘control number’
  3.   Baada ya kupatiwa ‘control’ namba atalipia Tsh 500/= kwa njia ya mtandao
  4.  Baada ya kufanya malipo atatakiwa kwenda kituo chochote cha Polisi kwa ajili ya uthibitisho
  5.   Baada ya kukamilisha hatua zote mwombaji ataprinti fomu hiyo kwa wakati wake.
Kwa kuanzia, mfumo huu wa utoaji wa fomu ya upotevu kwa njia ya mtandao umeanza kufanya kazi katika mikoa ya Dar es Salaam  na Pwani kama majaribio na ifikapo mwezi Juni, 2019 mfumo huo utatumika nchi nzima.

Jeshi la Polisi nchini  linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika mapambano dhidi ya uhalifu kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili kuendelea kudumisha  amani na usalama wa nchi yetu.

Imetolewa na:
…………………………………
Ahmed Z. Msangi – DCP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi.

Post a Comment

0 Comments