habari Mpya


TAKUKURU Yabaini Madudu Miradi ya Maendeleo Kigoma.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Kigoma imefanikiwa kuchunguza na kubaini manunuzi hewa ya vifaa ya ujenzi na usimamizi mbovu wa miradi minane yenye thamani ya shilingi bilioni 1.9 inayotekelezwa katika halmashauri na wilaya za mkoa huo.


Taarifa hiyo imetolewa na mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoani Kigoma Bw.Raphael Mbwambo wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kwa kipindi cha mwezi January hadi March mwaka huu 2019 ambapo hapa anabainisha miradi iliyofanyiwa uchunguzi sambamba na kilichobainika.

MBWAMBO.Katika hatua nyingine Bw.Mbwambo ameeleza kuwepo kwa miradi mbalimbali yenye thamani ya shilingi bilioni 8.9 iliyokwama kwa kipindi kirefu na kwamba taasisi hiyo inaanza uchunguzi wa miradi hiyo ili wahusika waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

MBWAMBO.


Kwa upande wake Mkuu wa dawati la elimu kwa umma TAKUKURU mkoani Kigoma Bi.Leonida Mushema amesema ili kukomesha vitendo vya rushwa mkoani humo wananchi katika maeneo yao hawana budi kuunga mkono juhudi za taasisi hiyo.

MUSHEMA

Post a Comment

0 Comments