habari Mpya


Nani kucheka, nani kulia? Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2019.

Hatimaye makundi sita ya mchuano wa Kombe la Mataifa ya Africa, Afcon 2019 yamepangwa.

 Kwa ukanda wa Afrika Mashariki, kwa vyoyote vile habari kubwa kwa sasa ni Kundi C ambalo linaundwa na Mataifa jirani ya Kenya na Tanzania.

Mataifa hayo, yanaungana pamoja na vigogo wa mpira wa Afrika mataifa ya Senegal na Algeria.

Kwa upande wa Uganda wao wapo Kundi A pamoja na wenyeji Misri, DR Congo na Zimbabwe.

Burundi wapo kwenye Kundi B pamoja na Nigeria, Madagascar na Guinea.

MAKUNDI YALIVYO. 
Fainali hizo za AFCON 2019 ,kwa mara ya kwanza mwaka huu 2019 zinashirikisha jumla ya timu 24 kutoka 16 zilizokuwa zinashiriki miaka ya nyuma.

 AFCON 2019 itaanza June 20,2019 kwa mchezo wa ufunguzi ukiwa kati ya mwenyeji  Misri  dhidi ya Zimbabwe na kumalizika July 19,2019.

Post a Comment

0 Comments