habari Mpya


Makamu wa Raisi Samia Hassan Suluhu Mgeni Rasmi Kongamano la Kimataifa la Biashara Kigoma.

Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo wameandaa kongamano la kimataifa la kibiashara linalotarajia kufanyika mkoani humo kwa kuzihusisha nchi Tano zinazolizunguka Ziwa Tanganyika lengo likiwa ni kuinua na kukuza uchumi wa mkoa na Taifa kwa ujumla.

Akitoa taarifa ya kongamano hilo , Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia General Mstaafu Emmanuel Maganga amesema zipo fursa nyingi za kimaendeleo katika mkoa huo ambazo kupitia kongamano hilo zitatambulika na kuwezesha kupatikana kwa soko la kudumu ndani na nje ya nchi.

MSIKILIZE HAPA RC MAGANGA.

Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa ameyataja baadhi ya matarajio kupitia kongamano hilo kuwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano ya ujirani mwema baina ya wafanyabiashara wa nchi za maziwa makuu.

BOFYA HAPA KUMSIKILIZA RC MAGANGA.
Kwa upande wao afisa biashara wa mkoa wa Kigoma Bw. Deogratius Sangu pamoja na Mwenyekiti wa jukwaa la wafanyabiashara TCCIA mkoa wa Kigoma Bw.Ramadhan Gange wameipongeza serikali kwa hatua hiyo ambayo itafungua fursa za kibiashara kwa wananchi wa mkoa huu na nchi za jirani.

WADAU

Aidha Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika May 9 hadi May 11 mwaka huu kwa kuzihusisha nchi za Kongo DR, Zambia, Rwanda ,Burundi na mwenyeji Tanzania huku Makamu wa Raisi wa Tanzania Samia Hassan Suluhu akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Post a Comment

0 Comments