habari Mpya


Halmashauri Tungeni Sheria Kuwabana Wananchi Wanaoshindwa Kutumia Vyandarua Kwa Matumizi Sahihi.

Wananchi wakishiriki Elimu juu ya Kudhibiti Ugonjwa wa Maralia.

Na Tunu na Amos -RK Mwanza na Kakonko.

Pamoja na Tafiti za hivi karibuni kuonyesha kuwa kiwango cha maambuki ya Ugonjwa wa Malaria kitaifa kinaendelea kushuka na kufikia asilimia 7.3, kwa mkoa wa Mwanza bado ni ya kiwango cha asilimia 8.1.

Kila ifikapo April 25 ya kila mwaka Tanzania huungana na mataifa mengine dunani kuadhmisha siku ya Malaria duniani, siku hii ikiwa mahsusi kupanga mikakati ya pamoja ya kupunguza au kutokomeza ugonjwa huo.

Mganga mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dr THOMAS RUTACHUNZIBWA amesema changamoto zinazochangia kuongezeka kwa ugonjwa wa malaria ni mapoja na imani potofu.

THOMAS RUTA CHUZIBWA.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza CRISTOPHAR  KADIO amesema mikakati ya Serikali ni kuhakikisha ugonjwa wa malaria unapungua au kuisha kabisa.
Katika Hatua nyingine, Mkuu wa wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Kanali HOSEA NDAGALA ameiagiza Halmashauri ya Wilaya hiyo kutunga sheria ndogo ndogo za kuwabana Wananchi wanaoshindwa kutumia vyandarua kwa matumizi sahihi.  

Akizungumza Katika maadhimisho ya siku ya maralia yaliyofayika kimkoa wilayani Kakonko amesema kuwa licha ya Serikali kuweka jitihada za kupambana na maralia bado baadhi ya wanachi wanatumia vyandarua wanavyo pewa kujengea mabanda ya kuku na wengine wakifunga nyumba zao ili zisinyunyiziwe dawa ya ukoko .

DC NDAGALA

Post a Comment

0 Comments