Na Faraja Marco -RK Kahama 97.3.
Askari Polisi
wa kituo cha Polisi wilaya ya Kahama H1363
PC Gideon Clement (30) mkazi wa Muleba mkoani Kagera, amejiua kwa kujipiga
risasi shingoni wakati akiwa kwenye lindo katika benki ya Access mjini Kahama.
Kamanda wa Polisi
mkoa wa Shinyanga, ACP RICHARD ABWAO amesema tukio la kujiua kwa Askari
huyo limetokea Alhamis Aprili 4,2019 majira ya saa moja na nusu asubuhi akiwa
eneo la kazi.
Kamanda ABWAO
amesema sababu za askari huyo kujiua ni kutokana na kutofanikiwa kupata mtoto
licha ya kuishi kwenye ndoa kwa muda wa miaka mitano na wamekuta ujumbe kwenye
simu aliokuwa akiwasiliana na mke wake kabla ya kutekeleza tukio hilo.
…….
Aidha
taratibu mbalimbali zinaendelea ili kuusafirisha mwili wa marehemu kwenda
kijijini kwao Muleba kwa ajili ya mazishi huku akiwasihi watumishi wa idara
mbalimbali kuepuka kujichukulia maamuzi wenyewe pindi wanapokumbwa na matatizo.
|
0 Comments