habari Mpya


Waziri Mkuu Majaliwa Kuzindua Soko Kuu la Dhahabu Mkoani Geita March 14, 2019.

Muonekano wa nje wa Ofisi za Soko la Dhahabu Geita ambalo limegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 2.

Na Gibson Mika –RK Geita.

Wafanyabiashara wa Madini ya Dhahabu Mkoani Geita wanatarajia kunufaika na biashara hiyo kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa soko kuu la Dhahabu.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robart Gabriel  katika kikao na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa soko hilo litasaidia kufungua fursa nyingi za uwekezaji kwa vijana na wanawake  kukuza uchumi wa taifa kupitia biashara za madini.

Pia amesema mbali na uwepo wa soko hilo, uongozi wa mkoa unaendelea na  ujenzi wa masoko madogo manane katika miji midogo katika mkoa huo kwa lengo la kuwakutanisha wachimbaji wadogo na wanunuzi wa dhahabu.

HAPA MSIKILIZE RC ROBART GABRIEL AKIZUNGUMZA.
Kwa upande wao baadhi ya Wachimbaji Mkoani Geita wamesema soko hilo litawapa uhuru wa kufanya kazi zao kwa kuwa litawakutanisha na wanunuzi wa dhahabu kutoka katika mataifa mbalimbali na kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya madini. 

Uziduzi wa soko hilo unatarajiwa kufanyika March 14, 2019, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.

Post a Comment

0 Comments