habari Mpya


Taswira Picha ya Bondia Hassan Mwakinyo akijifua kwa Pambano la March 23,2019.

Bondia Mtanzania HASSAN MWAKINYO bado anaendelea kujifua nchini Uingereza katika Jiji la Liverpool kwa ajili ya maandalizi ya pambano lake la March 23,2019 litakalofanyika nchini Kenya.

  HASSAN MWAKINYO baada ya kufanya vizuri pasipo kuwa na udhamini alipewa udhamini na SportPesa kama balozi wao kwa ajili ya kumsaidia kupata mafunzo kwa ufanisi na vifaa.
Akiwa nchini Uingereza , HASSAN MWAKINYO amepata fursa ya kufanya mazoezi au maandalizi ya pambano lake la March 23, kutoka kwa bondia wa Uingereza TONY BELLEW ambaye nae amewahi kufanya vizuri katika mapambano mbalimbali, na  hivyo MWAKINYO  kupata fursa ya kuboresha kipaji chake. 
Bondia HASSAN MWAKINYO alipata mafanikio makubwa mwezi September 2018 baada ya kumpiga bondia Muingereza SAM EGGINGTON kwa kumpiga Technical Knock Out  round ya 2 katika pambano la round 10.

Post a Comment

0 Comments