habari Mpya


Shinyanga Mwenyeji Siku ya Wanawake Duniani Leo March 8,2019.

Katika Kuelekea  Siku ya wanawake Duniani tarehe 08.03.2019 Wilaya ya Shinyanga imepewa kupaumbele Kuadhimisha Siku hiyo Kwa Mkoa wa Shinyanga.

Tanzania itaungana na Nchi Nyingine Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa tarehe 8, Machi ya kila mwaka,ambapo  dunia hukumbuka  mchango wa Mwanamke katika kufikia maendeleo kuanzia ngazi ya familia na taifa kwa ujumla.

Kauli Mbiu ya mwaka huu 2019 inasema ‘’BADILI FIKRA KUFIKIA USAWA WA KIJINSIA KWA MAENDELEO ENDELEVU’’.

Imeelezwa kuwa kupitia Sherehe Hiyo kwa Mkoa wa Shinyanga akina Mama wamekuwa na mwamko mkubwa kwa kufanya Shunguli mbalimbali za kijamii katika kuelekea kilele cha Siku hiyo.

SAMWELI LUCAS amezungumza na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi JACINTA MBONEKO ili kujua Mwamko wa akina mama katika Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani.

SIKILIZA HAPA CHINI ZAIDI.

Post a Comment

0 Comments