habari Mpya


Serikali Yaipa Miezi 3 Mikoa Ambayo Haikufikia Lengo Viwanda.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Mhe.  SELEMAN JAFO,akimkabidhi cheti cha ushindi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.ANTONY MTAKA baada ya mkoa wake kufanya vizuri katika kutekeleza ujenzi wa viwanda kwa kipindi kinachoishia Desemba 2018.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),  Mhe.SELEMAN JAFO,akimkabidhi cheti cha ushindi Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi ROBERT GABRIEL baada ya mkoa wake kufanya vizuri katika kutekeleza ujenzi wa viwanda kwa kipindi kinachoishia Desemba 2018.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),  Mhe.SELEMAN JAFO,akimkabidhi cheti cha ushindi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. BINILITH MAHENGE baada ya mkoa wake kufanya vizuri katika kutekeleza ujenzi wa viwanda kwa kipindi kinachoishia Desemba 2018.
Muwakilishi wa Mkuu wa Mikoa nchini, Mhe.AGREY MWANRI,akitoa shukrani kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),  Mhe.SELEMAN JAFO,akisema yeye na wakuu wa mikoa wenzake watahakikisha wanayachukua  maagizo hayo na kuyatekeleza kikamililifu ili adhima ya serikali iweze kukamilika.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),  Mhe.SELEMAN JAFO akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa viwanda mia moja (100) kwa kila mkoa kwa kipindi kinachoishia desemba 2018.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),  Mhe.SELEMAN JAFO akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Tawala  wa Mikoa baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa viwanda mia moja (100) kwa kila mkoa kwa kipindi kinachoishia desemba 2018.

Picha na Alex Sonna-Dodoma.
…………………………….
WaziriI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI,  Mhe.SELEMAN JAFO amesema hajapendezwa na baadhi ya mikoa ambayo haikufikia malengo waliyowekewa ya kujenga viwanda si chini ya mia moja 100, kila mkoa kwa mwaka.

Waziri JAFO aliyasema hayo March 19,2019 Jijini Dodoma, wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa viwanda mia moja (100) kwa kila mkoa kwa kipindi kinachoishia desemba 2018.

Waziri JAFO alisema hakufurahishwa na mikoa hiyo ambayo haikufikia malengo hayo, na kuwapa mda hadi kufikia MWEZI WA SITA MWAKA HUU,2019 kuhakikisha wanafikia malengo waliyowekewa na Serikali, ingawa hakuweza kuweka wazi mikoa hiyo ambayo haikufikia lengo.
Waziri JAJO alisema hakufurahishwa na mikoa hiyo kwa kutofikia lengo walilowekewa na serikali kuhakikisha inatekeleza mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano wa mwaka 2016/2017 -2020/2021 unaojikita katika ujenzi wa uchumi wa viwanda, ambao kwa kuanza kila mkoa ulitakiwa kuanzisha viwanda mia moja.

Waziri Jafo alibainisha kuwa hadi kufikia Desemba 31, 2018 viwanda vilivyokuwa vimejengwa kwa nchi nzima vilifikia elfu nne mia saba sabini na saba, (4,777) sawa na asilimia 183.73 ya lengo la kujenga viwanda 2,600 alisema licha ya  baadhi ya mikoa kuto kufikia lengo lakini kwa ujumla mikoa ilifanya vizuri.

Alisema viwanda hivyo viligawanywa katika makundi manne ambayo ni viwanda vikubwa 108, viwanda vya kati 236, viwanda vidogo ni 2,422, na viwanda vidogo kabisa ni 2,010, ambavyo vilikuwa vimetoa ajira kwa wananchi 36,796 kwa nchi nzima.

Aidha JAFO aliutaja mkoa wa DARE ES SALAAM kuwa ndio mkoa ulioongoza kwa upande wa mikoa iliyofanikiwa kujenga viwanda vikubwa ambao, ulijenga viwanda vikubwa arobaini na sita (46) kati ya viwanda mia moja na nane (108) vilivyojengwa nnchi nzima.

Ukifuatiwa na mkoa wa PWANI uliojenga viwanda nane 8, na nafasi ya tatu ikishikwa na mikoa mitatu ambayo ni MWANZA, LINDI NA SIMIYU ambayo kila mmoja ulijenga viwanda vikubwa saba (7).
Alisema Mikoa na Serikali za mitaa wanawajibu wa kuwatumia kikamilifu wataalamu hasa Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa Biashara na Wagani waliopo wanaopatikana katika maeneo yao ili kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda na upatikanaji wa malighafi za kutosha kwa ajiriya viwanda hivyo.

Pia aliwataka Watanzania kuhamasika kutumia bidhaa zinazozalishwa ndani ili adhima hiyo ya serikali ya ujenzi wa viwanda na kulinda ajira za watanzania katika viwanda ambavyo bidhaa hizo zinatoka.

Ikumbukwe  tarehe 9, novemba, 2017, Jijini Dodoma serikali  ilizindua kampeni ya ujenzi wa viwanda katika mikoa  na mamlaka za serikali za mitaa kote nchini ikiwa na kauli mbiu ya “MKOA WETU, VIWANDA VYETU”  ikiwa na lengo la kukuza uchumi katika kuelekea nchi ya kipato cha kati, na iliwaelekeza wakuu wa mikoa kila mmoja anaanzisha viwanda mia moja kwa mwaka.

Post a Comment

0 Comments