habari Mpya


Serikali Haimuonea Mvuvi Nchini.

Katika picha Waziri wa Mifugo na Uvuvi LUHAGA MPINA akiwasha moto kuteketeza nyavu zinazotumika katika uvuvi haramu Mjini Kigoma hivi karibuni -PICHA NA MAKTABA YETU. 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi LUHAGA MPINA, amesisitiza kuwa hatua zinazochokuliwa na Serikali za kudhibiti uvuvi usiofaa nchini hazilengi kumuonea mtu yoyote bali kuwalinda na maradhi sugu yatokanayo na uvuvi huo ukiwemo ule wa kutumia sumu.

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika mikutano ya kuwasilikiza wavuvi katika maeneo ya Kivinje na Somanga wilayani Kilwa mkoani Lindi, Waziri MPINA amesema hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano zimelenga kuwezesha kuwepo kwa rasilimali za kutosha za uvuvi. 

…….LUHAGA MPINA

Mmoja wa wavuvi wa Somanga wilayani Kilwa, MOHAMED KIMBWEMBE amesema wavuvi wengi wamekuwa wakijihusisha na uvuvi usiozingatia utaratibu kutokana Serikali zilizopita kushindwa kuchukua hatua.

…….MVUVI

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, CHRITOPHER NGUBIAGAI amemshukuru Waziri MPINA kwa kufika kuzungumza na wananchi hao, kwani ametoa ufafanuzi ambao utaoondoa sintofahamu iliyokuwa imetanda miongoni mwa wavuvi na kuwaomba kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kulinda rasilimali hizo za uvuvi.

Post a Comment

0 Comments