habari Mpya


Polisi Kagera Waua Washukiwa Watatu wa Ujambazi, Wakamata Silaha -Biharamulo.

Askari wa kikosi maalum kinachopambana na matukio ya uhalifu na wahalifu kama wanavyoonekana pichani wakitekeleza majukumu yao katika eneo la Midaho wilayani Biharamulo mkoani Kagera. 

Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza na askari wa kikosi maalum cha kupambana na matukio ya uhalifu na wahalifu katika eneo la Midaho wilayani Biharamulo mkoani Kagera 29/10/2018. Picha na Jeshi la Polisi.

Jehi la Polisi mkoani Kagera limewauwa kwa kuwapiga risasi watu watatu wanao dhaniwa kuwa majambazi baada ya majibizano ya kurushiana risasi baina ya polisi na watu hao katika kijiji cha Nyamaragara kata ya Lusahunga wilayani Biharamulo.

Kamanda wa polisi  mkoani Kagera REVOCATUS MLIMI akiwa  eneo la tukio la Kirakacheusi kijiji cha Nyamaragara  amesema tukio hilo limetokea  March 16,2019, saa tatu usiku na jeshi la polisi limefanikiwa kukamata silaha  aina ya A.K 47 na Magazine yenye risasi 17 .

Kamanda Mlimi amewataja marehem hao kuwa ni SHABANI  MANGOTEMA  mwenye umri wa miaka 40 mkazi wa Midaho  wilayani biharamulo, ERICK  SAMSON miaka 19 mkazi wa Benaco ambaye anadai wa raia wa Burundi na mwingine  jina lake bado halijafahamika.

KAMANDA MLIMI

Hata hivyo Kamanda Mlimi amewataka Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwajeshi la polisi pale watakapowatilia shaka  watu wasiowajua ili wakamatwe na kuchukuliwa hatua.

Post a Comment

0 Comments