habari Mpya


Mkuu wa Mkoa Shinyanga Azitaka Halmashauri Zote za Mkoa huo Kupanda Miti.

Kahama na Faraja Marko
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi.Zainabu Telaki amezitaka halmashauri zote za mkoa huo kusimamia kikamilifu zoezi la upandaji miti ili kuhifadhi mazingira ya mkoa huo.
Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Kahama baada ya kufanya ziara katika maeneo yote ya mkoani Shinyanga na kuona ongezeko kubwa la uharibifu wa Mazingira tofauti na kasi ya upandaji miti

Amesema kwa mjibu wa maelekezo ya serikali kila halmashauri inapaswa kupanda miti milioni 1 na laki 5 kwa kila mwaka nakwamba baadhi ya halmashauri zimeshindwa kutekeleza maagizo hayo

Naye Afisa Mazingira wa halmashauri ya mji wa Kahama Bw.Charlse Mwebesa amesema tatizo la uharibifu wa mazingira linatoka na shughuri za kibinadam ikiwemo uchomaji wa mkaa hivyo nivyema wananchi wakaacha kufanya hivyo badala yake waanze kupanda miti ili kutunza Mazingira.

Post a Comment

0 Comments