habari Mpya


Jamii Endeleeni Kusaidia Wasiojiweza Nchini.

Na Felix Baitu –RK Ngara.
Jamii nchini imeombwa kuendelea kujitolea kuwasaidia watu wasiojiweza katika maeneo yao ili kupunguza umaskini kwa kuanzia ngazi za familia.

Akizungumza March 19,2019 katika Jubilei ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Upendo la Masista wa KALIKUTA Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara mkoani Kagera, Mkuu wa Shirika hilo SISTA STANZIA amesema bado jamii ina mwamko mdogo katika kuwasaidia wahitaji.
SR.STANZIA
Aidha Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara SEVERINE NIWEMUGIZI pichani ameishukuru Serikali na Jamii kuendelea kuunga mkono shirika hilo la KALIKUTA ambao wanasaidia watu wenye mahitaji maalumu wakiwemo watoto na walemavu.

ASKOFU NIWEMUGIZI

Shirika la Masista wa KALIKUTA lilianza kufanya kazi ya kusaidia jamii ya watu wenye mahitaji maalumu wilayani Ngara mkoani Kagera mwaka 1994.

Post a Comment

0 Comments