Droo ya CAF
Champions League 2018/2019.
Wekundu wa
Msimbazi Simba SC ya Tanzania, itamenyana
na TP Mazembe ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba SC ambayo iliwakilishwa na Mwenyekiti, SWEDI NKWABI
na Mtendaji Mkuu, CRESCENTIUS MAGORI Katika droo hiyo, itaanzia
nyumbani kati ya Aprili 5 na 6,2019 kabla ya kusafiri kwenda Lubumbashi kwa
mchezo wa marudiano Aprili 12 au 13,2019.
Katika droo
iliyopangwa March 20, 2019 ukumbi wa Aida Ballroom, Marriot Zamalek mjini
Cairo, Misri, washindi wa kwanza wa Kundi D, Al Ahly ya Misri watamenyana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, CS Constantine ya Algeria itamenyana na Esperance ya Tunisia huku Horoya ya Guinea wakicheza na Wydad Casablanca ya Morocco.
Hapa chini ni Droo ya Kombe la CAF Confederation Cup
2018/2019.
|
0 Comments