habari Mpya


Waziri Mkuu Majaliwa Aagiza Kuimarishwa Ulinzi katika wilaya za Kibondo na Kakonko mkoani Kigoma.


Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza kuimarishwa kwa ulinzi katika wilaya za Kibondo na Kakonko mkoani Kigoma ili kukomesha ujambazi na utekaji katika maeneo hayo ambapo pia ametoa onyo kwa wahamiaji ambao wamekuwa wakiingia bila kuzingatia taratibu za uhamiaji.

Akiwa mkoani Kigoma, Waziri Mkuu ametembelea kambi ya wakimbizi ya Nduta iliyopo wilayani Kibondo na kuzungumza na wakimbizi.

Waziri Majaliwa aliwasili Mkoani Kigoma February 16,2019  kwa ziara ya siku 4 ikilenga kuweka mkazo na msisitizo katika ufufuaji na uendelezaji wa zao la chikichi ikiwa ni pamoja na  kukagua vitalu, mashamba, ili kufanya uboreshaji wa zao hilo.

Pia amepokea na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 ya CCM kwenye miradi mbalimbali pamoja na kuzungumza na wananchi katika maeneo atakayokuwa anakutana nao.

Post a Comment

0 Comments