habari Mpya


Waziri mkuu kufanya ziara ya siku nne mkoani Kigoma

Picha na Maktaba yetu.
Waziri Mkuu,wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Bw.Kassim Majaliwa anatarajia kufanya ziara ya kikazi mkoani Kigoma.

Waziri majaliwa atawasili mkoani humo kuanzia kesho februari 16,2019  kwa ambapo atakuwa mkoani humo kwa muda wa siku nne
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga amesema Majaliwa atatembelea wilaya ya Kigoma,Uvinza, Kibondo na Kakonko.

Amesema lengo la ziara yake hiyo ni kuweka mkazo na msisitizo katika ufufuaji na uendelezaji wa zao la chikichi ikiwa ni pamoja na  kukagua vitalu, mashamba, ili kufanya uboreshaji wa zao hilo.

Amesema akiwa mkoani humo Waziri Mkuu atatembelea kambi ya wakimbizi ya Nduta iliyopo wilayani Kibondo na kuzungumza na wakimbizi.

Amebainisha kuwa pamoja na mambo mengine ataangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 ya CCM na kukagua miradi mbalimbali pamoja na kuzungumza na wananchi katika maeneo atakayokuwa anakutana nao.

Post a Comment

0 Comments