habari Mpya


Wazazi na wanafunzi mkoani Geita waandamana wakishinikiza shule Mpya ya Rubondo mkoani humo ifunguliwe.

GEITA na Gibson Mika
Wananchi wa Kitongoji cha Mchangani kijiji cha Ihumilo kata ya Nkome wilaya ya Geita wameandamana hadi kwenye shule Mpya ya Rubondo wakiishinikiza serikali kuanza kusajili watoto wao baada ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kukamilika.

Hatua hiyo imekuja baada ya siku chache Mwanafunzi wa darasa la pili wa shule ya msingi Ihumilo kufariki kwa ajali ya kugongwa na pikipiki wakati akitoka shule hali iliyozua taharuki kubwa kwa wakazi wa kijiji hicho
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ihumilo na Mwaloni walioshiriki maandamano hayo wamesema kuwa hutembea mwendo mrefu kufika katika shule hizo na kwamba wakati mwingine huchelewa kutoka shule kutokana adhabu wanazopewa na walimu wao baada ya kuchelewa kufika shuleni.
Nao baadhi ya viongozi wa kata hiyo akiwemo Diwani wa kata Bw.Masumbuko Nsembe  na Afisa elimu kata ya Nkome Manda Keya, wamesema vyoo na mbao za kufundishia wanafunzi bado havijakamilika na kwamba kwa kushirikina na wananchi wanatarajia kukamilisha ndani ya wiki hii ili utaratibu mpya utangazwe.

Post a Comment

0 Comments