habari Mpya


Ubovu wa miundo mbinu ya umeme mkoani Kigoma wasababisha hasara hii

Kigoma na Adrian Eustace
Uwepo wa mifumo mibovu ya umeme na vifaa vinavyotumia umeme katika mkoa wa Kigoma vimetajwa kuwa chanzo cha majanga ya moto nakusababisha hasara kwa watumiaji wa umeme huo.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Jeshi la zima moto na uokoaji mkoani Kigoma Bw.Malumbo Ngata wakati akitoa mikakati ya kukabiliana na majanga ya moto kwa mwaka 2019.
Aidha amewataka wananchi wanaofunga vifaa vya umeme majumbani bila kufuata taratibu zilizowekwa na shirika la ugavi la umeme Tanesco kuacha mara moja kwani ni kuhatarisha maisha ya familia zao

Hata hivyo baadhi ya wananchi mkoani Kigoma wamesema ni vema elimu ya kukabiliana na majanga ya moto ianze kutolewa Shuleni ili iwafikie wananchi hao kwa urahisi zaidi.


Post a Comment

0 Comments