habari Mpya


Simba SC yaendeleza Wimbi la Ushindi Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara,Simba SC imefikisha pointi 48 baada ya kucheza mechi 19, sasa ikizidiwa pointi mbili tu na Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwa pointi zake 50 za mechi 25, wakati Yanga SC inaendelea kuongoza kwa pointi zake 61 za mechi 25.

Simba walicheza mechi yao ya Ligi February 26,2019 mjini  Iringa katika uwanja wa Samora  dhidi ya Lipuli FC ikiwa ni muendelezo wa michezo yao ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019 na kuwafunga wenyeji Lipuli  FC bao 3-1.

Magoli ya Simba SC yakifungwa na CLOTOUS CHAMA dakika ya 6, 44 na MEDDIE KAGERE dakika ya 58.

Lipuli FC waliopo nafasi ya 5 katika msimamo wa Ligi Kuu goli lao pekee lilifungwa na PAUL NONGA dakika ya 18 wakiwa na point 38 walizopata katika michezo yao 28.

Post a Comment

0 Comments