habari Mpya


Serikali za Vijiji Hakikisheni Majosho ya Kuogeshea Mifugo Yanafanya Kazi wakati Wote.

Wananchi wakishuhudia Ng'ombe akitoka kwenye Josho lililozinduliwa wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru  Picha na Maktaba.

Januari 15, 2019, Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilianza kampeni ya kitaifa ya uogeshaji mifugo katika kanda nane baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, LUHAGA MPINA Desemba 2018  wilayani Chato ikilenga kudhibiti magonjwa yaenezwayo na kupe.
Waziri MPINA alisema lita 10,232.53 za dawa aina ya Paranex (alphacypermethrin) ya kuua kupe zenye thamani ya Sh milioni 347 zimetolewa katika awamu ya kwanza. 

Halmashauri zote nchini zitaogesha mifugo kwa miezi sita mfululizo. Kanda ya kwanza ni ZVC Arusha- Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga; kanda ya pili ni Dodoma - Kati inayojumuisha mikoa ya Dodoma na Singida. Kanda ya tatu ni Iringa - Nyanda za Juu Kusini inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Njombe, Songwe, na Ruvuma wakati kanda ya nne ni Mtwara - Kusini inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara. Kanda ya tano ni Mwanza- Ziwa inayojumuisha mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Geita na Kagera huku kanda ya sita ikiwa ni Sumbawanga - Kusini Magharibi inayohusisha mikoa ya Rukwa na Katavi. Kanda ya saba ni Tabora - Magharibi inayojumuisha mikoa ya Tabora na Kigoma na kanda ya mwisho ni Temeke - Mashariki (Pwani na Morogoro). 
Takwimu za Wizara,kuna majosho 1,409 yanayofanya kazi huku majosho mengine 1,019 yasiyofanya kazi na inaelezwa kwamba kuna majosho mengi ambayo yanashindwa kufanya kazi ya kuogeshea mifugo kutokana na wananchi kufanya shughuli za kibinaadamu karibu na majosho hayo.

Hayo ni kwa mujibu wa Sr ROSAMISTIKA SAMBU, Daktari wa mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kanda ya ziwa wakati akizungumza na Redio Kwizera juu ya uhamasishaji unaofanywa na wizara kwa wafugaji kuogesha mifugo yao.

Sr. SAMBU amesma kutokana na ziara wanayoifanya ya kuzungukia majosho ndani ya halmashauri mbalimbali, wamegundua kuna wafugaji wanashindwa kuogesha mifugo yao kwa kuhofia kuingia migogoro na wakulima wanaolima karibu na majosho.
MSIKILIZE HAPA SR. ROSAMISTIKA

Kufuatia hali hiyo, amezitaka halmashauri kupitia serikali za vijiji kupitia sheria za vijiji kuhakikiha majosho hayo yanakuwa wazi kwa ajili ya uogeshaji wa mifugo pekee ili kupambana na kupe.

Post a Comment

0 Comments