habari Mpya


Serikali kununua zao la Parachichi nchini

Serikali imesema itaanza kununuas zao la parachichi nchini ili kuinua uchumi wa wakulima wanalima zao hilo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango Dakt.Philip Isdor Mpango baada ya kukutana na Wakulima na Wawekezaji wa zao la parachichi katika Wilaya ya Rungwe, Mkoani Mbeya.
Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa nchi,Ofisi ya Waziri mkuu anayeshughulikia Uwekezaji,Bi.Angela Kairuki na wataalam kutoka taasisi mbalimbali za Serikali na wadau wote wa zao la Parachichi nchini.

Waziri Mpango amesema Serikali ya awamu ya tano,imelenga kujenga uchumi wa viwanda unaoendana na maendeleo ya Sekta ya Kilimo,katika mkakati wa Pili wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo,nakwamba Serikali imeweka msukumo mkubwa kwenye mazao yenye thamani kubwa ikiwepo zao la parachichi.
 


Post a Comment

0 Comments