habari Mpya


Mweka Hazina Kibondo asimamishwa Kazi.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. KASSIM MAJALIWA amemsimamisha kazi Mweka Hazina wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, – THOMAS CHOGOLO, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma  zinazomkabili za ubadhilifu wa makusanyo ya mapato ya halmashauri hiyo.

Waziri Mkuu MAJALIWA ametangaza uamuzi huo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya  kikazi mkoani Kigoma.

 Amesema kuwa amefanya uamuzi huo kufuatia taarifa kuwa wananchi wa halmashauri hiyo ya wilaya ya Kibondo  wamekua wakilipa kodi kupitia kwa watendaji wa kata katika maeneo yao, lakini  Mweka Hazina huyo amekua haingizi kwenye mfumo wa Serikali,  jambo ambalo halikubaliki.

MSIKIE MAJALIWA HAPA AKIZUNGUMZA.

Katika hatua nyingine, Waziri  Mkuu KASSIM MAJALIWA, ameamuru kufungwa kwa Soko la Nduta na kuagiza lihamishiwe ndani ya kambi ya wakimbizi ili kuhibiti wa Wakimbizi wanaotoka nje ya kambi kwa ajili ya kupata mahitaji kwani hawatakiwi kuchanganyika na raia.

MSIKIE MAJALIWA HAPA AKIZUNGUMZA

Post a Comment

0 Comments