habari Mpya


Mamba Aua Mtoto wa Miaka 7 Muleba.

Wananchi wa Kijiji cha Katembe Kata ya Nyakabango wilayani Muleba mkoani Kagera wakitazama picha ya Mamba aliyeuliwa na Wananchi kwa kushirikiana na Ofisi ya  Maliasili na Wanyama Pori baada ya Mamba huyo kuua Mtoto IBRAHIM FESTO  miaka 7 na mwili wake ukiwa bado haujapatikana.

Picha/Habari Na Shafiru Yusuf –RK Muleba.

Mtoto IBRAHIMU FESTO miaka 7 amefiriki baada ya kuuliwa na Mamba katika mwalo wa ziwa victoria kijiji cha Katembe Kata ya Nyakabango Wilayani Muleba Mkoani Kagera na mwili wake bado haujapatikana hadi sasa.

Diwani wa kata ya Nyakabango Bw. PASTORI GWANCHELE ameiambia Redio Kwizera kuwa tukio hilo limetokea February 13, mwaka huu na mtoto huyo alikuwa anasoma darasa la pili katika shule yamsingi Muungano, ambapo siku ya tukio alikuwa na watoto wenzake watatu ambapo walikuwa wanafuata maji mwaloni ndipo mtoto huyo alivutwa na Mamba.

MSIKILIZE DIWANI HAPA CHINI.

Jeshi la Polisi wilayani Muleba kwa kusaidiana na Ofisi ya Maliasili na  Wanayama pori pamoja na Wananchi bado wanaendelea kuutafuta mwili wa mtoto huyo na leo wamefanikiwa kumuua mamba mmoja katika mwalo wa Magarini.

Post a Comment

0 Comments