habari Mpya


Maadhimisho ya Wiki ya Sheria wilayani Muleba.

Na Shafiru Yusuf -RK Muleba.

Mahakama ya wilaya ya Muleba mkoani Kagera imejipanga kuhakikisha inatoa elimu ya sheria mbalimbali kwa wananchi ili waweze kupata haki zao.

Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya muleba Bi. ASHA MWETINDWA amesema  hayo kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya sheria nchini iliyofanyika February 1, 2019 hii katika ukumbi wa mahakama ya wilaya ya Muleba.

Amesema kuwa tayari umewekwa  utaratibu wa kutembelea kila kata pamoja na shule za misingi na sekondari  wilayani humo kwa ajili ya kutoa elimu ya sheria mbalimbali.
Nao baadhi ya wananchi waliokuwa kwenye maadhimisho hayo wamesema kuwa licha ya kutoa elimu kwa wananchi bado baadhi yao wanachangamoto ya kufahamu Kwa kina zaidi juu  ya sheria mbalimbali  hivyo wameshauri kutolewa elimu ya mara kwa mara kwenye jamii hasa maeneo ya vijijini. 

Aidha kilele cha maadhimisho ya  siku ya sheria nchini inatarajiwa kufanyika February 6 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments