habari Mpya


Fahamu historia ya Marehemu Maria Philbert

Historia Fupi ya Marehemu

Marehemu Maria Philbert alizaliwa tarehe 9/12/1984 katika hospitali ya Aghakan jijini Mwanza, ni mtoto wa pili kati ya watoto watatu wa familia ya Bw. & Bi. Philbert Francis

Alisoma elimu ya msingi katika shule ya msingi Pamba (1993-1999) kisha akajiunga katika shule ya Sekondari Bulima (2005-2008).

(2009-2010) alijiunga na chuo cha Rayal Prince Training Centre wilayani Sengerema mkoani Mwanza na baadae akaanza kufanya kazi na redio Kwa neema FM Mwanza, mpaka mwaka 2012 kama mtangazaji wa kituo hicho
Mnamo Aprili 04 mwaka 2013 alijiunga na kufanya kazi na kituo cha Redio Kwizera FM iliyopo wilayani Ngara mkoani Kagera ambapo mpaka mauti yanamfika alikuwa mfanyakazi wa kituo hiki akitokea jijini Mwanza
Safari ya Kifo chake
Ilikuwa Januari 10 Marehemu Maria Philbert alianza kupata maumivu ya Kichwa yaliyosababishwa na Uvimbe sehemu ya kichwa ambapo Januari 19, 2019 alifanyiwa upasuaji mdogo akaendelea kupatiwa matibabu hatimaye akafariki Februari 16, 2019 siku ya Jumamosi saa 12: jioni
Maria ameacha mtoto mmoja wa kiume (Philbert Francis)
Wakati wa uhai wake Marehemu amewahi kupata tuzo ya umahiri wa uandishi wa habari zilizoandaliwa na taasisi ya Building Nutrition Food basket project Tanzania.
Familia inawashukuru waandishi wa habari wa Mwanza, Redio Kwizera, ndugu, jamaa na marafiki wote walioshiriki mazishi ikiwemo kutoa faraja kwa wafiwa kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments